Unyanyasaji wa Kingono kwenye Sehemu za Kazi

Sheria ya kazi na mahusiano ya kazi ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa maboresho mwaka 2019, imezungumzia kidogo sana juu wa unyanyasi wa kingono kwenye sehemu za kazi. Sheria imeweka unyanyasaji wa kingono chini ya makundi au aina ya ubaguzi mahala pa kazi na hivyo kuonekana kama ni tatizo dogo sana kwenye eneo la kazi na mahusiano ya kazi.

Kumekuwa na matatizo mengi sana juu ya tatizo hili la unyanyasaji wa kingono kazini, watu wengi sana wamekuwa wakinyanyaswa na watu mbalimbali ikiwemo waajiri au hata wafanyakazi wenzao na hivyo kusababisha matatizo makubwa sana kwao ikiwemo msongo wa mawazo.

Katika kipindi chetu cha leo kama ilivyo ada, tupo na Dada Chiku Semfuko, ambaye ni Mwanataaluma kwenye maswala ya kinjisia. Chiku amebahatika kufanya kazi sehemu mbalimbali juu ya maswala ya kazi hususan masuala ya unyanyasaji wa kingono kazini. Katika kipindi chetu cha leo tunazungumza nae kinagaubaga juu ya swala hili, ukubwa wa tatizo na nini kifanyike kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii yetu kwa ujumla.

Kuhusu watoa mada:

Chiku Semfuko

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Title
.